• HABARI MPYA

    Thursday, April 19, 2012

    ARTETA AMEMALIZA MSIMU ARSENAL

    Arteta
    KIUNGO Mikel Arteta atakosa mechi zote zilizobaki za Arsenal msimu huu kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu, vyombo vya habari Uingereza vimesema katika taarifa iliyoifikia bongostaz.blogspot.com.
    Kiungo huyo wa Hispania, ambaye alitoa mchango mkubwa kwa mafanikio ya Arsenal siku za karibuni, aliumia kifundo cha mguu wakati akipiga krosi mwanoni mwa mechi ya Jumatatu waliyofungwa 2-1 na Wigan Athletic Uwanja wa Emirates.
    Arteta alitibiwa uwanjani – wakati huo Wigan wamefunga bao lao la pili – lakini hakuweza kuendelea na mchezo.
    Vipimo vinaonyesha kifundo hicho cha mguu hakijavunjika, lakini ameumia sana na maumivu yake yatamuweka nje ya Uwanja na kukosa mechi nne za ligi ambazo Arsenal imebakiza.
    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye timu yake itamenyana na Chelsea nyumbani Jumamosi, sasa ana pengo kubwa katika safu ya kiungo kwani tayari anawakosa majeruhi wa muda mrefu Jack Wilshere na Abou Diaby.
    Yossi Benayoun, anayecheza kwa mkopo kutoka Chelsea, hataruhusiwa kucheza mechi hiyo kwa mujibu wa mkataba wake.
    Arsenal inashika nafasi ya tatu, ikiwazidi pointi tano wapinzani wao, Tottenham Hotspur ambao wana mchezo mmoja mkononi.
    Baada ya kumenyana na Chelsea mwishoni mwa wiki hii, Arsenal itacheza na Stoke Cit ugenini, kisha Norwich City  nyumbani na kumaliza na West Bromwich Albion.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARTETA AMEMALIZA MSIMU ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top