• HABARI MPYA

    Sunday, April 01, 2012

    RONALDO ATUPIA MAWILI, MESSI MOJA REAL, BARCA ZIKISHINDA LA LIGA

    Ronaldo kulia
    MABAO ya Andres Iniesta dakika ya 39 na Lionel Messi kwa penalti dakika ya 57 usiku wa jana yalitosha kuipa Barcelona ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye Uwanja wa Camp Nou.
    Kwa sababu Real Madrid nay ilishinda 5-1 dhidi ya Osasuna, Barcelona bado wanazidiwa pointi sita na vinara hao wa La Liga katika msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania.
    Cristiano Ronaldo aling’ara wakati Real Madrid ikiitandika 5-1 Osasuna wakati Matajiri hao wa Madrid wakitimiza mabao 100 msimu huu.
    Ronaldo alifunga mabao mawili dakika ya 36 na 69, wakati Benzema alifunga dakika ya sita, Higuain dakika 39 na 76 na bao la kufutia machozi la Osasuna lilifungwa na Nino dakika ya 47.
    Real ya kocha Mreno, Jose Mourinho sasa ina pointi 78, na imekaribia mno taji lao la kwanza la ubingwa wa la Liga ndani ya miaka minne dhidi ya Barca ambao sasa wana pointi 72.
    Malaga wanaoshika nafasi ya nne walifungwa 2-0 nyumbani Real Betis na kuendelea kulingana kwa pointi (47) na Valencia, ambao wanacheza leo. Osasuna ipo nafasi ya sita kwa pointi zake 43 na Bilbao ya kocha Marcelo Bielsa ya 11 kwa pointi zake 38.
    Ronaldo jana alifikisha mabao 37 na kwa mabao ya Karim Benzema na Gonzalo Higuain pia, Real ilipata ushindi wa kwanza katika La Liga Pamplona tangu wawe mabingwa mwaka 2008.
    Real Zaragoza iliendeleza jitihada zake za kuepuka kushuka daraja kwa ushindi wa tatu mfululizo, ikiibwaga 2-1 Sporting Gijon. Racing Santander ilifungwa 1-0 nyumbani na Granada bao la dakika ya 89 la penalti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO ATUPIA MAWILI, MESSI MOJA REAL, BARCA ZIKISHINDA LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top