• HABARI MPYA

    Thursday, April 09, 2009

    YANGA YAIZAWADIA POINTI TATU AZAM, YAJIEPUSHA NA BALAA LA KUHSUKA DARAJA


    AZAM imetoka kifua mbele baada ya kuifunga Yanga mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Mabao mawili ya Boniphace Ambani yaliyomfanya kufikisha mabao 16, yalifutwa na Yahaya Tumbo aliyefunga mawili na Shaaban Kisiga na kuifanya Azam kujiongezea pointi tatu na kufikisha pointi 25 na hata kulikimbia janga la kushuka daraja.
    Mchezo huo ulioanza taratibu kwa pande zote kufanya mashambulizi ya hapa na pale, japokuwa haukuwa na mashambulizi ya hapa na pale.
    Yanga ilikuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya 27 lililowekwa kimiani na Ambani kwa shuti kali baada ya kuwachambua mabeki wa Azam na kuachia kombora lililompita kipa, Vladmir Niyonkini. Dakika 11 baadaye, Mike Baraza akiwa na kipa huyo, alipaisha mpira.
    Hapo kabla, dakika ya 20, Philip Arando aliachia fataki lililodakwa na Juma Kaseja na dakika tatu baadaye Osmund Monday alikosa bao baada ya Kaseja kupangua shuti lake.
    Azam ilishambulia kwa nguvu na katika dakika ya 39, mwamuzi Oden Mbaga aliwapa Azam penalty baada ya Arlando kuangishwa ndani ya eneo la hatari, lakini hata hivyo, Kaseja alipangua penalti ya Monday.
    Yanga ilifunga bao la pili katika dakika ya 43, kupitia kwa Ambani baada ya kupata krosi ya Baraza.
    Kipindi cha pili Azam walifanya mabadiliko kwa kumtoa Alando na kumuingiza Yahaya Tumbo ambaye aliipatia Azam bao la kwanza katika dakika ya 54 kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa kichwa wa Danny Wagaruka.
    Dakika sita baadaye, Shaaban Kisiga aliisawazishia timu yake kwa kichwa baada ya kuunganisha wavuni kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Wagaruka.
    Katika dakika ya 66, Tumbo aliipatia timu yake bao la tatu baada ya kuachia mkwaju uliopanguliwa na Kaseja na kumkuta tena akaukwamisha wavuni.
    Azam walipata penalti katika dakika ya 80 baada ya Castory Mumbala kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari lakini Kisiga akakosa penalti hiyo iliyopanguliwa na Kaseja. Hata hivyo, Azam ilipata pigo dakika mbili baadaye baada ya Nsa Job kulimwa kadi nyekundu. Awali alionyeshwa kadi ya njano.
    Kocha wa Azam, Itamar Amourin alisema timu yake imecheza vizuri na walijua kuwa watashinda mchezo huo kutokana na ari ya wachezaji wake.
    Kocha wa Yanga, Dusan Kondic aligoma kuzungumzia mchezo huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAIZAWADIA POINTI TATU AZAM, YAJIEPUSHA NA BALAA LA KUHSUKA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top