• HABARI MPYA

  Monday, April 13, 2009

  EEH MUNGU MFUNGULIE NJIA NYOTA HUYU...

  Winga wa Yanga mwenye kasi na chenga za maudhi, Mrisho Khalfan Ngassa aliondoka jana kwenda Uingereza kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya West Ham United ya huko. Ngassa, mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba ya Dar es Salaam, aliondoka na wakala wake Yussuf Bakhresa kwenda kujaribu bahati yake. bongostaz inamtakia kila la heri mchezaji huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EEH MUNGU MFUNGULIE NJIA NYOTA HUYU... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top