• HABARI MPYA

    Saturday, April 04, 2009

    SIMBA KUENDELEZA UBABE KWA KAGERA?

    Haruna Moshi 'Boban' wa Simba katika moja ya mechi za timu yake, ataibeba timu yake Kaitaba?

    SIMBA ya Dar es Salaam, kesho inashuka kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kumenyana na Kagera Sugar katika mchezo uliobeba taswira kubwa ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.Mshindi katika mchezo wa leo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, atakuwa amejitengenezea mazingira mazuri ya kukabidhiwa tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).Simba inashuka dimbani kesho, ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 18 sawa na Kagera yenye pointi 28, zote zikiwania nafasi ya pili kwenye ligi hiyo, ambayo tayari ubingwa wake umekwishachukuliwa na Yanga.Kihistoria, Simba ndio wababe wa Kagera, kwani imekuwa ikiwafunga kila msimu tangu imepanda Ligi Kuu mwaka 2005. Kagera imeifunga Simba mara moja tu kwenye Ligi, hiyo ilikuwa mechi ya kwanza tangu ipande Mei 25, mwaka 2005.Zaidi ya hapo, Kagera iliifunga tena Simba kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Tusker mwaka 2006.Mara ya mwisho zilipokutana mjini Dar es Salaam, Oktoba 14, mwaka jana Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa, bao pekee la mshambuliaji chipukizi Moses Godwin Mwazembe katika dakika ya 19, lilitosha kuwapa Wekundu wa Msimbazi ushindi wa 1-0.Simba itashuka dimbani leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-0 iliyoupata dhidi ya Azam FC mjini Dar es Salaam Jumatatu, hivyo leo itakuwa pia na nia ya kuendeleza wimbi lake la ushindi, wakati wapinzani wao, Kagera Sugar wanakumbuka kipigo cha 1-0 kutoka Prisons na baadaye sare ya 1-1 na Yanga.Safu ya ushambuliaji ya Simba kama kawaida inaweza kuongozwa na wakali wake Emeh Izuchukwu, Mohamed Kijuso, Ulimboka Mwakingwe bila kumsahau kipenzi cha Wekundu wa Msimbazi, Haruna Moshi ÔBobanÕ.Langoni hapana shaka kocha Patrick Phiri anaweza kuendelea kumuanzisha kipa aliye vizuri hivi sasa kimchezo, Ally Mustafa ÔBarthezÕ atakayesaidiwa na mabeki Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Meshack Abel na kiungo wa ulinzi Juma Nyosso.Kagera yenyewe kama kawaida lango lake linaweza kuwa chini ya ulinzi wa Odo Nombo, atakayekuwa akilindwa na mabeki mahiri kama Bakari Omar, wakati safu ya kiungo itaongozwa na Paul Kabange na kwenye ushambuliaji kama kawaida, mfungaji bora wa msimu uliopita Mike Katende atakuwa akiiongoza.
    REKODI YA SIMBA NA KAGERA:

    MEI 25, 2005: Simba Vs Kagera Sugar 0-1

    MFUNGAJI: Shingwe Mussa dakika ya 67

    SEP 28, 2005

    Kagera Sugar Vs Simba 0-2

    WAFUNGAJI: Mussa Mgosi dk 21, Nico Nyagawa dk 35

    JUNI 3, 2006:

    Kagera Sugar Vs Simba 0-1

    (Hata hivyo, Oktoba 30, mwaka huo, Kagera ilizawadiwa ushindi wa 2-0 na pointi tatu za chee, Simba ikidaiwa kumtumia Mussa Mgosi aliyekuwa na kadi tatu za njano)

    OKTOBA 18, 2006:

    Simba Vs Kagera Sugar 2-1

    KOMBE LA TUSKER 2006;

    Fainali; Agosti 20, Uwanja wa Taifa

    Simba Vs Kagera Sugar 1-2 (dakika 120)

    WAFUNGAJI: Emmanuel Gabriel dk. 80; Omary Changa dk. 90, 97)

    OKT. 13, 2007

    Simba Vs Kagera Sugar 2-1

    WAFUNGAJI: Simba: Moses Odhiambo dk 6 (penalti), Ulimboka Mwakingwe dk. 54;

    KAGERA: Vincent Barnabas dk. 11

    APRIL 19, 2008

    Kagera Sugar Vs Simba 0-1

    MFUNGAJI: Ramadhani Chombo dk. 24

    OKTOBA 14, 2008

    Simba Vs Kagera 1- 0

    MFUNGAJI: Moses Godwin dk. 7
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA KUENDELEZA UBABE KWA KAGERA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top