• HABARI MPYA

    Friday, April 10, 2009

    MISS UTALII WATANGAZA TENDA...



    WAANDAAJI wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania, kampuni ya Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant na kamati ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania,wametangaza kuwa wanatoa nafasi kwa makampuni,taasisi na watu binafsi kujitokeza kudhamini fainali za kumsaka mrembo wa Miss Utalii Tanzania mwaka 2009.
    Fainali za mwaka huu zimepangwa kuanza Mwanzoni mwa mwezi Juni 2009 katika ngazi za Majimbo,Wilaya,Mikoa,Kanda na kufikia kilele chake kwa fainali za Taifa kufanyika Octoba 2009.
    Kwa miaka mitano sasa tumekuwa tukiendesha mashindano haya kwa kutumia nguvu na rasilimali zetu kwani udhamini ambao tumekuwa tukiupata haukuwa ukifikia hata robo ya bajeti ya kuendesha mashindano.Hata hivyo katika kipindi chote kigumu cha miaka mitano cha kuendesha mashindano haya kwa ukata,tumeweza kuwadhihirishia si watanzania tu bali ulimwengu kwa ujumla kuwa uwezo,nia,sababu na ujuzi wa kuendesha mashindano ya urembo kwa mafanikio makubwa na ya pekee tunao.
    Tunaomba wadhamini wajitokeze kwani Mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania ndiyo pekee yenyemafanikio makubwa nay a kujivunia kuliko mengine yoyote hapa Tanzania na ukanda wa Afrika ya Mashariki na kati.Mafanikio hayo ni pamoja na:
    Ø Kuwa Mashindano ya kwanza katika historia ya Tanzania kabla na baada ya uhuru kutwaa taji la Dunia,pale Miss Utalii Tanzania 2004,Witness Manwingi alipoitoa Tanzania kimasomaso kwa na kukomesha Tanzania kuwa kichwa cha mwenda wazimu katika mashindano ya urembo Dunia pale alipo twaa taji la Dunia la Miss Tourism World Africa 2005.
    Ø Kuwa ndiyo mashindano pekee nchini kutwaa mataji ya dunia kila mwaka tulioshiriki mashindano ya Dunia,kwa miaka minne mfululizo tangu 2005 baada ya kutwaa taji la Dunia huko katika fainali zilizo fanyika Harare Zimbabwe,taji la pili la Dunia ni Miss Utalii Tanzania 2006 Killy Janga alipo twaa taji la dunia la Miss Tourism world SADIC 2006 katika fainali za dunia zilizo fanyika Taipei China,taji la tatu ni pale Miss Utalii Tanzania 2007 Lytha Syprian alipotwaa taji la dunia la Miss Tourism World Bikini Africa 2007 katika fainali za Dunia zilizo fanyika Antalya Uturuki,taji la nne ni pale Lily Shirima mshindi wa pili wa Miss Utalii Tanzania 2005 alipotwaa taji la dunia la Miss Tourism World Internet Africa 2006 katika fainali zilizo fanyika Great Britain ,taji la tan ni pale Miss Utalii Tanzania tena alipotwaa taji la Miss Afrika 2005 katika shindano lililofanyika Addis Ababa Ethiopia ,baada ya kuteuliwa na wizara ya Habari Michezo na Utamaduni kuwakilisha Tanzania na taji la sita ni pale mrembo huyo wa Miss Utalii Tanzania alipotwaa taji la Miss Tourism Model Of The World Personality 2006 katika fainali za dunia zilizo fanyika Tanzania 2006.
    Ø Kuwa ndiyo mashindano ya kwanza kufanikiwa kuwashawishi waandaaji wa Dunia kuiteua Tanzania kwa mara ya kunza kuwa wenyeji wa fainali za dunia na kushirikisha nchi zaidi ya 100.
    Ø Kuwa ni miongoni mwa Mashindano machache nchini ambayo yanasura halisi ya kitaifa kwa kufanya fainali zake kuanzia ngazi za Majimbo,Wilaya,Mikoa na Kanda kila mwaka bila ya kukosa tangu kuanzishwa kwake ,hivyo kuwa na wawakilishi wa kila mkoa tangu kuanzishwa kwake 2004.
    Ø Kuwa ndiyo mashindano pekee ambayo yanatangaza vivutio vya utalii na utamaduni wa mtanzania kimataifa na kitaifa,hivyo kuwa hazina na benki kubwa ya utamaduni wa mtanzania kwa manufaa ya sasa na baadae ya Tanzania na watanzania.
    Tunaamini kuwa mafanikio haya na mengine mengi ambayo hatujayataja ni kielelezo dhabiti kuwa,wakati sasa umefika ,tena wakati sahihi kwa watanzania,makampuni na mashirika binafsi nay a umma ya kizalendo nay a kigeni kutuunga mkono kwa hali na mali ili tuweze kufanya makubwa zaidi kwa manufaa ya Taifa,watanzania na wadhamini watakaojitokeza.
    Tumejiwekea malengo kuanzia mwaka huu kulifanya shindano hili kuwa ndilo bora zaidi hapa nchini na Duniani kwa ujumla,tumedhamilia kutwaa taji la Dunia yani la Miss Tourism world 2009 na la Miss World Heritage 2009 baada ya mfululizo wa mataji ya miaka ya nyuma ili kuandika na kubadilisha historia ya mashindano ya urembo nchini kwa mara nyingine.Kikwazo kwetu cha kufikia malengo haya ni kukosa udhamini unaofikia angalau asilimia 60% ya au hata 50% bajeti ya mwaka.Hakika tunaomba wadhamini wajitokeze ili ndoto ya kutwaa mataji makuu ya dunia yaweze kutimia.
    Katika kuhakikisha hayo yanafanyika ,tumeimarisha uongozi na kamati ya Taifa kwa kuteua wajumbe wenye uzoefu na uwezo mkubwa katika fani ya Michezo na urembo kitaifa na kimataifa pia tumechukua hatua ya kuimarisha ngazi za mawakala wa mikoa ,wilaya,kanda na majimbo. Kubwa zaidi ni kwamba tayari tumeingia makubaliano na moja ya kituo kikubwa cha televisheni na redio mbili nchini amcho kitarusha matangazo ya moja kwa moja mashindano yote ya mikoa,kanda na Taifa,huki matangazo ya mashindano hayo yakifanyika na kujumuisha wadhamini kwa siku 21 kabla ya kila shindano la ngazi husika katika Televisheni na Redio,hii itatoa fulsa ya pekee kwa wafanyabiashara makampuni na watoa huduma mbalimbali kujitangaza karibu bara zima la Afrika ambako televisheni na Redio hizo zinasikika kwa uhakika.
    Tunaomba wadhamini ambao wako tayari kudhamini fainali za ngazi yoyote wawasiliane na Rais wa Mashindano haya Gideon Chipungahelo,au wajumbe wa kamati ya taifa ambao ni pamoja na Henry Tandau mwenyekiti wa Kamati,venance Mwamoto Katibu wa Kamati,Sara Ramadhani Mjumbe,Dotnata (Husna Mohamedi) mjumbe,Tomas Bangu Mjumbe,Kinjikitile ngombalemwilu Mjumbe,bahati singh mjumbe na au mawakala wetu walioko mikoani na au Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). (pichani kushoto ni Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo 'Chips')
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MISS UTALII WATANGAZA TENDA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top