• HABARI MPYA

    Wednesday, December 31, 2025

    MLANDEGE WAVULIWA KOMBE LA MAPINDUZI MAPEMA TU

    TIMU ya Mlandege SC imevuliwa Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa bao 1-0 na URA ya Uganda katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Bao pekee la URA katika mchezo wa leo limefungwa na  mshambuliaji Fred Amaku na kwa kupoteza mchezo wa pili kufuatia kuchapwa mabao 3-1 na Singida Black Stars kwenye mchezo wa kwanza.
    Sasa Mlandege SC watakamilisha mechi zao za Kundi A kwa kumenyana na Azam FC Ijumaa ya Januari 2 hapo hapo New Amaan Complex.
    George Masembe wa URA amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi hiyo na kuzawadiwa Sh. Milioni 1 kutoka kwa wadhamini, Benki ya NMB Tanzania.


    Jamal Saleh Mchezaji wa Mlandege FC amechaguliwa Mchezaji Mwenye Nidhamu baada ya l mchezo huo na kuzawadiwa kiasi cha Shilingi 500,000 kutoka kwa wadhamini, Benki ya NMB Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MLANDEGE WAVULIWA KOMBE LA MAPINDUZI MAPEMA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top