• HABARI MPYA

    Wednesday, December 31, 2025

    AZAM FC NA SINGIDA BLACK STARS ZATOA SARE 1-1 MAPINDUZI


    TIMU za Azam FC na Singida Black Stars zimetoa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Azam FC walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake mpya, Mkongo Jephte Kitambala Bola, kabla ya mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Guede kuisawazishia Singida Black Stars.
    Kwa matokeo hayo, Singida Black Stars wanafikisha pointi nne kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Mlandege FC kwenye mchezo wa kwanza, wakati Azam FC iliyocheza mechi yake ya kwanza leo inaanza na pointi moja.
    Kiungo wa Azam FC, Himid Mao amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi na kuzawadiwa Sh. Milioni 1 kutoka kwa wadhamini, Benki ya NMB, wakati Abdulmalik Zakaria amezawadiwa Sh. 500,000 kwa Mchezaji kwenye Nidhamu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NA SINGIDA BLACK STARS ZATOA SARE 1-1 MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top