• HABARI MPYA

    Saturday, December 13, 2025

    SULEIMAN MWALIMU AONGEZWA TAIFA STARS


    WINGA wa Wydad Athletics ya Morocco anayecheza kwa mkopo Simba SC, Sumeiman Mwalimu ‘Gomez’ ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.
    Kocha  Muargentina, Miguel Angel Gamondi amemuongeza Mwalimu kwenye kikosi hicho kilichoweka kambi nchini Misri kuziba nafasi ya mchezaji wa Azam FC, Abdul Suleiman ‘Sopu’ ambaye ni majeruhi.
    Katika Fainali hizo za AFCON zinazotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21  hadi Januari 18, mwakani — Taifa Stars imepangwa Kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SULEIMAN MWALIMU AONGEZWA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top