• HABARI MPYA

    Monday, December 29, 2025

    PHIRI KOCHA MPYA WA MAKIPA SIMBA SC YA STEVE BARKER

    KLABU ya Simba imemtambulisha Mzambia, Davies Phiri (49) kuwa Kocha wake mpya wa makipa katika benchi jipya la Ufundi chini ya Kocha Mkuu, Steven Robert "Steve" Barker raia wa Afrika Kusini.
    Taarifa ya Simba katika kurasa zake imetambulisha na kumkaribisha Phiri, kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia ambaye anajiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea AmaZulu F.C. ya Afrika Kusini.
    “Karibu Simba SC, Kocha wa Makipa Davies Phiri,” imesema taarifa kwenye kurasa za Simba SC.
    Phiri kabla ya kuwa kocha amecheza sika ha kulipwa Afrika Kusini akidakia klabu za Durban Stars, Golden Arrows na Kabwe Warriors.
    Phiri alikuwepo kwenye kikosi cha Zambia kilichofika Nusu Fainali ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 1996 na kufungwa na Tunisia 4–2. 
    Alikuwepo pia kwenye kikosi cha Chipolopolo kilichoshiriki AFCON ya 1998 na kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi D Kiki am ULI’s pointi nne tu na mwaka 2000 pia walipomaliza nafasi ya tatu Kundi C na mwaka 2002 waliposhika mkia, nafasi ya Kundi D kwa kuambulia pointi moja tu.
    Akiwa Kocha mwaka 2011 alikuwa sehemu ya benchi la Ufundi la Zambia lililoiandaa timu kwa ajili ya AFCON ya 2012 ambazo walitwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti 8–7 dhidi ya Ivory Coast.
    Aidha,Simba imemtambulisha Prinil Deen, raia wa Afrika Kusini kuwa mchumbuzi wa video (Video analyst).
    “Karibu kwenye familia ya Simba SC, Mchambuzi wa Video,”. 
    Simba pia imemtambulisha Sibusiso Meshack Makhula kuwa Kocha wake mpya wa mazoezi ya utimamu ya mwili, (Fitness Coach) kutoka Upington City FC ya kwao, Afrika Kusini.
    Mtaalamu huyo mwenye Masters ya Sayansi ya Michezo aliyopata katika Chuo Kikuu cha Wits University tayari yupo nchini kwa ajili ya kwanza kazi chini ya Mkuu, Steve Barker.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PHIRI KOCHA MPYA WA MAKIPA SIMBA SC YA STEVE BARKER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top