WENYEJI, FC Barcelona jana walitoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Spotify Camp Nou Jijini Barcelona, Hispania.
Eintracht Frankfurt walitangulia kwa bao la winga wa kulia, Ansgar Knauff dakika ya 21, kabla ya beki wa kulia Mfaransa Jules Olivier Koundé mwenye asili ya Benin kuifungia mfululizo Barcelona dakika ya 50 na 53.
Kwa ushindi huo, Barca inafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya 14 kwenye ya timu 36 za Ulaya, wakati Eintracht Frankfurt inabaki na pointi zake nne nafasi ya 30 baada ya timu zote kucheza mechi sita.



.png)
0 comments:
Post a Comment