• HABARI MPYA

    Tuesday, December 09, 2025

    GAMONDI AFICHUA JESHI LAKE LA AFCON YA MOROCCO



    KOCHA Muargentina, Miguel Angel Gamondi ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 28 wa Taifa Stars kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025  zinazotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21  hadi Januari 18, mwakani.
    Taifa Stars imeweka kambi nchini Misri tangu jana kujiandaa na AFCON hadi Desemba 18 itakapoondoka kwenda Morocco tayari kwa Fainali hizo hizo za 35 za Kombe la Mataifa ya Afrika.
    Taifa Stars ambayo inashiriki Fainali hizo kwa mara ya nne baada ya 1980 Nigeria, 2019 Misri na 2023 Ivory Coast — imepangwa Kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda.
    Katika Fainali zote zilizotangulia Taifa Stars imekuwa ikitolewa hatua ya makundi - tena bila kushinda mechi hata moja wakitoa sare na kufungwa.
    Mwaka 1980 walifungwa 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri pamoja na Sara ya 1-1 na Ivory Coast, 2019 walifungwa mechi zote, 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria — wakati mwaka 2023 walifungwa mechi moja, 3-0 na Morocco na sare za 1-1 na Zambia na 0-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


    KIKOSI CHA MWISHO TAIFA STARS AFCON 2025
    Makipa; Yakoub Suleiman (Simba SC), Hussein Masalanga (Singida Black Stars) na Zuberi Foba (Azam FC).
    Mabeki; Shomari Kapombe (Simba SC), Wilson Nangu (Simba SC), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Pascal Msindo (Azam FC), Nickson Kibabage (Singida Black Stars), Haji Mnoga (Salford City, England), Dickson Job (Yanga SC), Ibrahim Abdulla ‘Bacca’ (Yanga SC), Bakari Nondo Mwamnyeto (Yanga SC) na Mohamed Hussein ‘Tshabalala (Yanga SC).
    Viungo; Novatus Dismas (Goztepe FC, Uturuki), Kelvin Nashon  (Pamba Jiji), Habibu Iddi (Singida Black Stars), Tarryn Allarakhia (Rochdale AFC, England), Charles Mombwa (Floriana FC, Malta), Morice Abraham (Simba SC), Feisal Salum Abdallah (Azam FC), Iddi Suleiman ‘Nado’  (Azam FC), Ahmed Pipino (KMC FC) na Alphonse Mabula (Shamakhi, Azerbaijan), Suleiman Mwalimu (Wydad AC Morocoo, mkopo Simba SC).
    Washambuliaji; Kibu Dennis (Simba SC), Kelvin John (Aalborg BK, Denmark), Simon Msuva (Al-Talaba, Iraq na Nahodha, Mbwana Samatta (Le Havre, Ufaransa).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GAMONDI AFICHUA JESHI LAKE LA AFCON YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top