• HABARI MPYA

    Saturday, December 27, 2025

    BENIN YAPATA USHINDI WA KWANZA AFCON, YAICHAPA BOTSWANA 1-0 AFCON


    TIMU ya Benin imeibuka na ushindi wa bao 1–0 dhidi ya Botswana katika mchezo wa Kundi D Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 jioni ya leo Uwanja wa Olimpiki Jijini Rabat nchini Morocco.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Shamirah Nabadda wa Uganda, bao pekee la Benin limefungwa na beki mzaliwa wa Ufaransa, Yohan Cédric Benjamin Roche wa Petrolul Ploiești ya Romania dakika ya 28.
    Kwa ushindi huo, Benin ambayo ilifungwa bao 1-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Katika mchezo wa kwanza inaokota pointi tatu katika mechi ya pili na kuweka hai matumaini ya kusonga mbele.
    Kwa upande wao Botswana baada ya kufungwa mabao 3-0 na Senegal kwenye mchezo wa kwanza inajiweka pagumu kusonga mbele. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENIN YAPATA USHINDI WA KWANZA AFCON, YAICHAPA BOTSWANA 1-0 AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top