• HABARI MPYA

    Tuesday, June 08, 2021

    WAWILI WAJITOKEZA KUMNG'OA WALLACE KARIA TFF, WACHUKUA NAYE FOMU LEO KUWANIA URAIS KATIKA UCHAGZI WA AGOSTI 7 TANGA

     

    WADAU wawili wamejitokeza kuwania Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Wallace John Karia anayeshikilia nafasi hiyo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 7 mwaka huu Jijini Tanga.
    Hao ni Evans Mgeusa na Zahor Mohamed Hajji ambao wote wamechukua fomu leo kwa gharama ya Sh. 500,000 pamoja na Karia.
    Zoezi la uchukuaji fomu linatarajiwa kuendelea hadi Jumamosi Saa 10:00 jioni makao makuu ya TFF, Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam au kupitia tovuti ya shirikisho hilo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAWILI WAJITOKEZA KUMNG'OA WALLACE KARIA TFF, WACHUKUA NAYE FOMU LEO KUWANIA URAIS KATIKA UCHAGZI WA AGOSTI 7 TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top