• HABARI MPYA

  Thursday, December 15, 2016

  SIMBA YAWATEMA AME ALI, AWADH NA SEMWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba imewatema wachezaji kadhaa wakiwemo beki Emmanuel Semwanza, kiungo Awadh Juma na mshambuliaji Ame Ali.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema leo kwamba marekebisho hayo madogo yanatokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu, Mcameroon Joseph Marius Omog.
  Manara amesema kwamba, Ame Ali aliyekuwa anacheza kwa mkopo kutoka Azam FC, amerejeshwa kwenye klabu yake hiyo, wakati Awadh Juma na Malika Ndeule wamepelekwa kwa mkopo Mwadui FC ya Shinyanga na Semwanza amekwenda Maji Maji FC ya Songea kwa mkopo pia.

  Ame Ali amerejeshwa kwenye klabu yake hiyo Azam FC 

  Aidha, Manara amethibitisha Simba kuachana rasmi na kipa Muivory Coast Vincent Angban na kiungo Mkongo, Mussa Ndusha. 
  Wakati hao wakiachwa, Simba SC ikmewasajili wachezaji wawili raia wa Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei na washambuliaji wazawa Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma Luizio anayekuja kwa mkopo kutoka Zesco ya Zambia.
  Mbali na kuachwa kwa wakongwe hao, klabu pia imewapandisha wachezaji wawili wa kikosi cha vijana, beki Vincent Costa na Nahodha na mshambuliaji Moses Kitandu 
  "Tunaamini maboresho haya yataongeza chachu ya ushindani ktk kikosi chetu na Hatimaye kutupa mataji msimu huu. Niwaarifu pia timu yetu imeondoka asubuhi hii kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda Fc, mchezo utakaopigwa Jumapili huko Mtwara,"alisema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAWATEMA AME ALI, AWADH NA SEMWANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top