• HABARI MPYA

    Thursday, December 01, 2016

    AZAM SASA YAFUATA VIPAJI KIGOMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    ZOEZI la klabu ya Azam FC kusaka vipaji vya wachezaji vijana chini ya umri wa miaka 17 wikiendi hii linahamia mjini Kigoma ambako litafanyika Jumamosi.
    Huo ni mwendelezo wa mpango wa Kitaifa wa timu hiyo wa kutengeneza kikosi imara cha timu ya vijana wa umri huo, ambapo inakwenda Kigoma kutokana na mkoa huo kuwa historia ya kisoka nchini ya kutoa wanasoka wengi waliotamba.
    Majaribio hayo ya pili kuelekea mwisho wa kufungwa zoezi hilo, yatafanyika ndani ya Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Jumamosi hii kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na vijana wanaotakiwa ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 2000 hadi 2004.
    Hadi sasa zoezi hilo limeshahusisha mikoa sita, ambayo ni Dar es Salaam, Tanga, Morogoro & Dodoma, Visiwani Zanzibar, Mbeya na Mwanza, ambapo kiujumla Azam FC imewafanyia usaili jumla ya vijana 3, 265 na kuvuna 70 pekee kati ya hao waliochaguliwa, huku 151 wakiwekwa akiba kwenye kumbukumbu za mradi huo.
    Vijana hao wote waliochaguliwa kwenye mikoa mbalimbali, wanasubiria kuitwa kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika ndani ya Uwanja wa Azam Complex baadaye mwezi huu Desemba, ambao ndio utatoa vijana bora watakaounda timu hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM SASA YAFUATA VIPAJI KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top