• HABARI MPYA

  Thursday, December 01, 2016

  SHIME KOCHA MPYA JKT RUVU, KIBADENI BADO MKUU WA BENCHI LA UFUNDI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Bakari Shime sasa ndiye kocha mpya wa timu ya JKT Ruvu Stars ya Pwani.
  Ofisa Habari wa JKT Ruvu, Costantine Masanja alisema jana kwamba, Shime ambaye msimu uliopita alikuwa JKT Mgambo ya Pwani, mara moja anaanza kazi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  JKT ambayo imeingia kambini Mbweni mwishoni mwa wiki kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu inahitaji kufanya kazi ya ziada kujiepusha na hatari ya kushuka daraja.
  Bakari Shime (kushoto) sasa ndiye kocha mpya wa timu ya JKT Ruvu Stars ya Pwani

  Kocha Msaidizi an anakuwa Koplo Alex Mwamgaya, kocha wa makipa, Aajini Abdalah Ngachimwa, wakati Makoplo George Minja na Amosi Mgisa wataendelea kuwa Makocha Wasaidizi waandamizi wa kikosi cha timu ya vijana chini ya miaka 20, chini ya Kocha Mkuu Koplo Azishi Kondo na Msaidizi wake Koplo Haruna Adolf.
  Mkongwe Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ anaendelea kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu zote za JKT Ruvu Stars, zikiwemo na za vijana na za wanawake.
  Kuhusu kusajili, au kutosajili dirisha dogo limeachiwa benchi la Ufundi kuamua na kwa kuanzia kocha Shime na benchi lake zima watawaangalia wachezaji wa kikosi cha U-20 na wachezaji wengine wanajeshi waliorejea kutoka kwenye kozi na majukumu mengine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHIME KOCHA MPYA JKT RUVU, KIBADENI BADO MKUU WA BENCHI LA UFUNDI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top