• HABARI MPYA

    Tuesday, March 17, 2015

    YANGA WAVUNA MILIONI 100 KASORO KIDOGO MECHI NA PLATINUM

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    MECHI ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC dhidi ya timu ya FC Platinum ya Zimbambwe iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam iliingiza mil 91,660,000 kutokana na watazamaji 14,563 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
    Mgawanyo wa mapato katika mchezo huo ni, VAT 18% sh. 13,982,033, Gharama ya tiketi sh. 12,380,000, Uwanja 15% sh. 9,794,694.92, Gharama za mchezo 15% sh. 9,794,694.92, TFF 5% sh. 3,264,898.31, CAF 5% sh. 3,264,898.31 na Young Africans 60% sh.39.178,779.66.
    Katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya michuano hiyo, Yanga SC ilianza kwa ushindi wa 5-1 nyumbani dhidi ya Platinum FC na sasa itakwenda kupigania hata sare ugenini wiki ijayo ili kusonga mbele.
    Salum Telela akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Platinum Jumapili

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAVUNA MILIONI 100 KASORO KIDOGO MECHI NA PLATINUM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top