CHELSEA imeshindwa kutumia fursa ya kupaa kileleni mwa Ligi Kuu England kwa point inane zaidi, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Southampton jioni ya leo Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Diego Costa alianza kuifungia The Blues akimalizia krosi ya Branislav Ivanovic dakika ya 11, kabla ya Dusan Tadic kusawazisha kwa penalti dakika ya 19, kufuatia Sadio Mane kuangushwa na Nemanja Matic.
Ivanovic alilalamika angestahili kupewa penalti kipindi cha kwanza baada ya kuangushwa na Tadic kwenye boksi. Blues sasa inaidizi kwa pointi Manchester City na ina mechi moja mkononi.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic/Ramires, Fabregas, Willian/Cuiadrado, Oscar/Ramires, Hazard na Costa.
Southampton; Forster, Clyne, Fonte, Alderweireld, Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, S. Davis/Ward-Prowse, Tadic/Djuricic, Mane na Long/Pelle.
Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa akiruka juu kuifungia timu yake katika sare ya 1-1 na Southampton
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2995830/Chelsea-1-1-Southampton-Dusan-Tadic-levels-Diego-Costa-opener.html#ixzz3UTZOg564


.png)
0 comments:
Post a Comment