TIMU ya Arsenal imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa sheria ya mabao ya ugenini, baada ya usiku wa kuamkia leo kushinda 2-0 dhidi ya Monaco ya Ufaransa.
Safari ya Arsenal katika michuano ya mwaka huu inaishia hatua ya 16 bora, baada ya awali kufungwa mabao 3-1 nyumbani, hivyo kufanya sare ya jumla ya 3-3.
Olivier Giroud aliifungia bao la kwanza Arsenal dakika ya 36, kabla ya Aaron Ramsey kutokea benchi kipindi cha pili na kufunga la pili dakika ya 79.
Manchester City ni timu pekee ya England iliyobaki kwenye michuano ya Ulaya, na yenyewe imekaa ‘mkao wa kutolewa’ na Barcelona.
Kikosi cha Monaco kilikuwa: Subasic, Fabinho, Wallace Santos, Abdennour, Kurzawa, Toulalan, Kondogbia, Joao Moutinho, Dirar/Echiejile dk86, Martial/Carrasco dk59 na Berbatov/Bernardo Silva dk70.
Arsenal: Ospina, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal/Gibbs dk83, Coquelin/Ramsey dk63, Cazorla, Ozil, Welbeck/Walcott dk72, Sanchez na Giroud.
Arsene Wenger akiwa amejiinamia na kushika kichwa baada ya Arsenal yake kmutolewa na Monaco Ligi ya Mabingwa Ulaya
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2999541/Monaco-0-2-Arsenal-agg-3-3-Olivier-Giroud-Aaron-Ramsey-goals-not-Gunners-crash-Champions-League.html#ixzz3UhKvSmio


.png)
0 comments:
Post a Comment