• HABARI MPYA

    Tuesday, October 28, 2014

    YAYA TOURE APAMBANISHWA NA RONALDO TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA, MESSI NDANI, SUAREZ NJE

    NYOTA watano wa Ligi Kuu ya England na Muingereza mmoja, Gareth Bale - wameorodheshwa katika majina 23 ya FIFA kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mwaka 2014, maarufu kama Ballon d'Or.
    Mchezaji anayeshikilia tuzo hiyo kwa sasa, Cristiano Ronaldo na mshindi mara nne wa tuzo hiyo, Lionel Messi kwa mara nyingine wanapewa nafasi kubwa ya kushindania ufalme wa kusakata kabumbu duniani.
    Lakini ajabu, mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez, aliyefungiwa miezi mitatu Julai mwaka huu kwa kumng'ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunia hayumo.
    Wachezaji sita walioshinda Kombe la Dunia katika kikosi cha Ujerumani, wameorodheshwa, huku wachezaji watano wanaocheza England walioingia ni pamoja na nyota watatu wa Chelsea, Eden Hazard, Diego Costa na Thibaut Courtois, wengine ni Mwafrika pekee Yaya Toure wa Manchester City na Muargentina wa Manchester United, Angel Di Maria. 

    Wazi kitendo cha Suarez kumng'ata Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunia kimemgharimu kutokuwemo orodha fupi ya wawania Ballon d'or licha ya kazi nzuri aliyoifanya msimu uliopita akiwa na Liverpool kabla ya michuano hiyo ya dunia.
    Kitabu cha mwongozo cha FIFA juu ya uteuzi wa wawania tuzo hiyo kinasema: "Kigezo cha uteuzi wachezaji wa mwaka (wanaume na wanawake) ni: kuangali uchezaji wake sambamba na nidhamu ndani na nje ya Uwanja kuanzia Novemba 30 mwaka 2013 hadiNovemba 21 mwaka 2014,". 

    WALIOTEULIWA KUWANIA BALLON D'OR 2014... 

    Gareth Bale (Wales), Karim Benzema (Ufaransa), Diego Costa (Hispania), Thibaut Courtois (Ubelgiji), Cristiano Ronaldo (Ureno), Angel Di Maria (Argentina), Mario Gotze (Ujerumani), Eden Hazard (Ubelgiji), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta (Hispania), Toni Kroos (Ujerumani), Philipp Lahm (Ujerumani), Javier Mascherano (Argentina), Lionel Messi (Argentina), Thomas Muller (Ujerumani), Manuel Neuer (Ujerumani), Neymar (Brazil), Paul Pogba (Ufaransa), Sergio Ramos (Hispania), Arjen Robben (Uholanzi), James Rodriguez (Colombia), Bastian Schweinsteiger (Ujerumani) na Yaya Toure (Ivory Coast).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE APAMBANISHWA NA RONALDO TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA, MESSI NDANI, SUAREZ NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top