• HABARI MPYA

    Friday, October 24, 2014

    KOCHA BARCA ATHIBITISHA SUAREZ ATACHEZESHWA DHIDI YA REAL MADRID KESHO

    KOCHA Luis Enrique bado anasuasua kufanya maamuzi mazito zaidi tangu aanze kazi Barcelona – kumuanzisha ua kutomuanzisha mshambuliaji Luis Suarez kesho dhidi ya Real Madrid, lakini amethibitisha atacheza japo kidogo.

    VIKOSI VYA KESHO CLASICO...

    Real Madrid: Casillas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Rodriguez, Modric, Kroos, Isco; Ronaldo na Benzema 
    Barcelona: Bravo; Alves, Pique, Mascherano, Mathieu; Rakatic, Busquets, Iniesta; Suarez, Messi na Neymar 
    Suarez amemaliza adhabu yake baada ya kumng'ata Mtaliano Giorgio Chiellini katika Kombe la Dunua la El Clasico ya kesho unatarajiwa kuwa mchezo wake wa kwanza wa mashindano tangu Julai. 
    Lakini kocha wa Barca amekataa kusema kama atamuanzisa au la, akisema; "Hapana, siwezi kucheza mechi hiyo leo,"amesema leo Enrique.
    Luis Enrique hajathibitisha kama Luis Suarez ataanza dhidi ya Real Madrid kesho 

    "Suarez atapata dakika za kucheza, lakini siwezi kusema kiasi gani,"amesema. "Hii ni nafasi kubwa kwake kujipambanua katika timu mpya. Dakika ngapi atapata, siwezi kusema,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA BARCA ATHIBITISHA SUAREZ ATACHEZESHWA DHIDI YA REAL MADRID KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top