![]() |
| Ronaldo ataibeba Real Jumatano? |
![]() |
| Messi ataendeleza maajabu yake kesho? |
WAKATI ikizidi kukaribiwa na Barcelona
kileleni, vinara wa Ligi Kuu ya Hispania, Real Madrid Jumatano wanakabiliwa na
mechi ngumu ya wapinzani wa jiji la Madird, dhidi ya Atletico Madrid inayopigana
kuvunja rekodi ya kucheza mechi 22 na wapinzani wao hao bila kushinda.
Sare tatu katika mechi tano
zilizopita, limeipunguzia Madrid kiwango cha pointi za kuongoza La Liga kutoka
10 hadi nne, na Barcelona itakuwa mchezo mwepesi tu kesho dhidi ya Getafe
nyumbani.
Madrid watasafiri hadi Uwanja wa
Vicente Calderon katika mchezo muhimu zaidi kushinda kuliko hata dhidi ya Barcelona
katika wiki zisizozidi mbili.
“Pengo na Barcelona limepungua, lakini
sasa tunatakiwa kuendelea kusonga mbele,” alisema Nahodha wa Madrid, Iker
Casillas.
“Mechi na wapinzani wetu itakuwa
maalum. Baada ya muda mrefu wa kutotufunga, kwao utakuwa mchezo muhimu sana
kwao.”
Atletico haijafunga Madrid tangu
mwaka 1999 na wanataka kurudi kile kilichofanywa na Valencia Jumapili kutoka
sare ya 0-0 na Real.
Kikosi cha Jose Mourinho, Madrid
hadi sasa kimefunga mabao mengi msimu huu, 100 — 74 kati ya hayo yanatokana na Cristiano
Ronaldo, Gonzalo Higuain na Karim Benzema—na wanaelekea kuvunja rekodi ya daima
ya mabao 107.
Messi amekwishafanya makubwa na
kuvunja rekodi kibao na kesho anatarajiwa kuwa mwiba kwa Getafe.
Jumamosi Messi alifunga mabao
mawili na kuweka rekodi nyingine, kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 60 katika
michuano mikubwa Ulaya, tangu Mjerumani Gerd Mueller afunge 67 alipokuwa Bayern
Munich msimu wa 1972-73.
Muargentina huyo anaongoza kwa
mabao La Liga, 38, moja tu zaidi ya Ronaldo, Mreno wa Real. Wote wanawania kuvunja
rekodi ya mabao mengi katika La Liga dhidi ya rekodi ya Ligi ya Ureno ya mabao 40
msimu uliopita.
Mechi nyingine kesho, Osasuna inayoshika
nafasi ya sita itakuwa mwenyeji wa Espanyol, wakati Real Betis itakuwa mgeni wa
Real Sociedad.
Valencia wanaoshika nafasi ya
tatu watajaribu kuendeleza maajabu yao Jumatano watakapocheza na Rayo
Vallecano, ikitoka kupigwa 6-0 na Osasuna mwishoni mwa wiki.
Levante itasaka pointi mbele ya Sporting
Gijon.
Mechi nyingine Jumatano, Athletic
Bilbao itaifuata Granada na Alhamisi Villarreal watamenyana na Malaga; Racing
Santander na Mallorca; na Sevilla dhidi ya Zaragoza.




.png)
0 comments:
Post a Comment