• HABARI MPYA

    Monday, April 09, 2012

    NEWCASTLE WAPAA ENGLAND, SPURS WAPIGWA NYUMBANI

    Kiungo Mfaransa wa Newcastle, Hatem Ben Arfa (wa pili kulia) akishangilia bao lake na beki wa England, Danny Simpson (kushoto), mshambuliaji wa England mwenye asili ya Nigeria, Shola Ameobi (wa pili kushoto) na kiungo wa Argentina Jonas Gutierrez (kulia).
    KLABU ya Newcastle imejiongezea matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, kufuatia ushindi wa tano mfululizo leo wakati Tottenham ikianza kupoteza matumaini baada ya kufungwa nyumbani.
    Mshambuliaji wa Newcastle, Papiss Cisse amefunga bao la 10 ndani ya mechi tisa tangu ajiunge na klabu hiyo Januari mwaka huu, na kusababisha ushindi wa 2-0 kwa Newcastle dhidi ya Bolton, baada ya Hatem Ben Arfa kufunga la kwanza.
    Ushindi huo unawainua The Magpies hadi nafasi ya tano, nyuma ya Tottenham kwa tofauti ya mabao tu, baada ya klabu hiyo ya London kuchapwa 2-1 na Norwich.
    Anthony Pilkington na Elliott Bennett waliifungia Norwich, ambayo inaangukia nafasi ya tisa sasa.
    Chelsea inaweza kupanda juu ya Tottenham na Newcastle kama itashinda mechi yake na Fulham inayoendelea hivi sasa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NEWCASTLE WAPAA ENGLAND, SPURS WAPIGWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top