![]() |
| Balotelli kulia na Tevez kushoto katika mechi ya Jumapili |
MSHAMBULIAJI wa Manchester City,
Mario Balotelli leo ameomba radhi mjini Milan kwa utovu wake wa nidhamu na ameomba
asiondolewa timu ya Taifa ya Italia kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Ulaya.
Alilimwa kadi nyekundu ya nne
katika misimu miwili akiwa na City timu yake ikilala 1-0 mbele ya Arsenal Jumapili,
jambo ambalo limeibua swali, huenda Balotelli amevunja agizo la nidhamu na
uadilifu lililowekwa na kocha wa Italia, Cesare Prandelli.
“Samahani sana kwa kilichotokea
kwa pigo nililoisababishia Manchester City, na maalum kwa (kocha) Roberto
Mancini, ambaye ninamzimikia na kumtakia mema,” Balotelli alisema katika
taarifa yake iliyotolewa na shirika la habari la ANSA na wakala wake, Mino
Raiola.
“Ninahusika sana katika timu ya
taifa, lakini jana nilicheza faulo mbili katika matukio ya mchezo, si kwa ugomvi.”
Balotelli alilimwa kadi nyekundu
dakika ya 90, baada ya kupewa kadi ya kwanza ya njano kwa kumchezea rafu Bacary
Sagna, dakika tatu baada ya Mikel Arteta kuifungia Arsenal.
“Sikuvunja kipengele cha uadilifu,”
alisema Balotelli. “Tayari nimekwishaikosa timu ya taifa kwa upumbavu na siwezi
kufanya hivi kwa mara ya pili.
Natumaini kuwapo katika kambi ya
mazoezi Aprili. Acha tusubiri hadi mwisho wa adhabu.”
Balotelli alifungiwa mechi nne
za Ligi Kuu Januari baada ya kumfanyia undava Scott Parker wa Spurs hali
iliyosababisha Prandelli amteme kwenye kikosi cha Itali kilichocheza mechi ya
kirafiki na Marekani Februari.
“Nitayafanyia tathmini (matukio
ya Balotelli) kwenye video juu ya kadi zake kama yanakiuka kipengele cha
uadilifu Balotelli,” alisema Prandelli leo, wiki mbili kabla ya kuanza kwa
kambi ya Italia.
Mbali na Balotelli, kiungo Daniele
De Rossi na mzaliwa wa Argentina, mshambuliaji Pablo Osvaldo pia walitoswa timu
ya taifa kwa sababu ya nidhamu tangu Prandelli atambulishe kipengele cha
nidhamu alipopewa timu ya taifa, mwaka 2010.
Baada ya mechi na Arsenal, kocha
wa City, Mancini alisema; “ilikwisha” na Balotelli.
“Namsikitia sana, kwa sababu
anapoteza kipaji chake na ubora wake,” alisema Mancini.
“Anelekea kubaya katika mustakabali
wake, na anatakiwa kubadili mwenendo wake.”



.png)
0 comments:
Post a Comment