• HABARI MPYA

    Wednesday, August 19, 2015

    MAREFA 'MAADUI' WA YANGA WAPEWA MECHI YA NGAO, KUNA NKONGO NA HASHIM ALIYECHEZESHA MECHI YA 5-0 ZA SIMBA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAREFA wawili ambao ‘hawatafutika’ katika kumbukumbu za machungu ya wana Yanga SC, Israel Mujuni Nkongo na Hashim Abdallah watachezesha mechi ya Ngao ya Jamii Jumamosi.
    Yanga SC itamenyana na Azam FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na leo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetaja marefa wa mchezo huo wa kuashiria upenuzi wa pazia la Ligi Kuu.
    Nkongo aliyewahi kupigwa na wachezaji wa Yanga SC Machi 10, 2012 timu hiyo ikifungwa 3-1 na Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumtoa kwa kadi nyekundu beki Nadir Haroub 'Cannavaro' akiwa tayari ametoa kadi nyekundu kwa kiungo Haruna Niyonzima pia. 
    Wachezaji wa Yanga SC wakimkimbiza Nkongo Machi 10, mwaka 2012 Uwanja wa Taifa 

    Stefano Mwasyika aliyehamia Ruvu Shooting alimtupia ngumi ya ‘kibondia’ Nkongo na Nadir Haroub ‘Canavaro’ alionekana kuhusika katika vurugu hizo wote wakafungiwa na TFF, enzi hizo Rais ni Leodegar Tenga. 
    Mashabiki wa Yanga SC walifanya vurugu kubwa na kuvunja viti Uwanja wa Taifa siku hiyo.
    Yamepita hayo na Nkongo amepewa tena mechi ya Yanga na atasaidiwa na Samuel Hudson Mpenzu wa Arusha, Josephat Daud Bulali wa Tanga, wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam na Kamisaa wa mchezo huo ni Deogratius Rwechungura kutoka mkoani Mara.
    Hashim alitoa penalti tatu kwa wapinzani, Mei 6, mwaka 2012 Yanga ikipigwa 5-0 na Simba SC, mabao ya Emmanuel Okwi mawili, Felix Sunzu, Juma Kaseja na Patrick Mafisango Jumamosi atakuwa mezani.
    Hashim Abdallah akimuonyesha kadi ya njano aliyekuwa kipa wa Yanga SC, Said Mohammed kabla ya kutoamoja ya penalti tatu, Yanga SC ikilala 5-0 Mei 6, mwaka 2012
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREFA 'MAADUI' WA YANGA WAPEWA MECHI YA NGAO, KUNA NKONGO NA HASHIM ALIYECHEZESHA MECHI YA 5-0 ZA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top