• HABARI MPYA

  Thursday, August 20, 2015

  MAGWIJI WA MUZIKI WAREKODI 'NGOMA' YA KUUTAKIA HERI UCHAGUZI MKUU 2015

  WIMBO maalum wa dansi wa kuuombea amani uchaguzi mkuu, unatarajiwa kusikika radioni hivi karibuni baada ya kurekodiwa katika studio za Sound Crafters, Temeke, jijini Dar es Salaam. 
  Mratibu wa umoja wa muda wa wasanii wa dansi na taarab, Juma Mbizo ameiambia Saluti5 kuwa wimbo upo katika hatua za mwisho na kwamba baadhi ya wapulizaji ala za upepo idara yao. 

  Mwinjuma Muumin akiwa studio wakati wa kurekodi wimbo huo

  Mbizo alisema wimbo huo ulioko katika miondoko ya rumba na uliopewa jina la “AMANI KWANZA” utaandaliwa video na kuanza kusambazwa kwenye vituo vya radio na luninga nchini kote. “Baadhi ya wanamuziki wa muziki wa dansi na taarab wameamua kuunda umoja wa muda na kurekodi nyimbo mbili za kuhamasisha amani kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25,” alisema Mbizo. 
  Wimbo wa pili utakuwa ni katika miondoko ya taarab ambapo tayari na wenyewe upo kwenye hatua za mwisho kabla haujaachiwa rasmi hewani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAGWIJI WA MUZIKI WAREKODI 'NGOMA' YA KUUTAKIA HERI UCHAGUZI MKUU 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top