Na Princess Asia, TANGA
KIKOSI cha Simba SC kimegoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kuelekea mchezo wao dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting.
Baada ya kufika Uwanja wa Mkwakwani majira ya 8:45 mchana kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba walikataa kwenda kwenye chumba cha walichopangiwa na wakaamua kubadilishia nguo kwenye basi lao.
Walipomaliza kubadilsiha nguo katika basi lao, waliteremka na kukaguliwa kabla ya kwenda kuanza kupasha misuli moto Uwanja wa Mkwakwani.
Tayari vikosi vya timu zote mbili vipo Uwanja wa Mkwakwani vikipasha misuli moto na kikosi cha Simba SC leo kipo hivi; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Abdi Banda, Said Ndemla, Ibrahim Hajibu, Emmanuel Okwi na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Mgambo Shooting; Godson Mmasa, Bashiru Chanache, Salim Mlima, Salim Kipanga, Ramadhani Malima, Novaty Lufunga, Mohammed Samatta, Ally Nassor, Fully Maganga, Malima Busungu na Salim Aziz Gilla.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni.

.png)
0 comments:
Post a Comment