Na Vincent Malouda, NAIROBI
KURUHUSIWA kwa kampuni inayosimamia ligi kuu Kenya, KPL, kuendelea na ligi yake kunaashiria ligi mbili kuu nchini Kenya.
Hii ni baada ya hakimu wa Mahakama kuu ya Kenya, Roselyn Ekirapa Aburili kutupilia mbali marufuku ya KPL kutoanda ngarambe zozote kwa mujibu wa maombi yaliyowasilishwa mahakamani na Shirikisho la Soka Kenya, FKF, ambalo halikutaka kampuni hiyo kusimamia ligi kuu msimu huu baada ya kutoelewana kuhusu idadi ya timu zitakazoshiriki ligi kuu.
Kutokana na hayo, FKF ilianzisha ligi yake kuu huku KPL ikisimamisha mechi zake majuma matatu yaliyopita kufuatia amri ya korti licha ya kucheza mechi za ufunguzi Februari 21 na 22.
Kwa majuma matatu sasa timu kumi na nne zikiwemo Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi hazijashiriki pambano lolote la ligi kuu zikisubiri uamuzi wa mahakama ambapo jaji Aburili aliwapa mashabiki wa soka kitu wanachopenda moyoni mchana wa leo.
Sasa ni rasmi ya kwamba ligi kuu itaendelea tangia ino Jumatano Nakuru AllStars wakiandaa zulia la Afraha kudananadana na Sofapaka kisha siku ya Alhamisi, Gor Mahia washikane mashati na Bandari ugani City.



.png)
0 comments:
Post a Comment