• HABARI MPYA

    Tuesday, March 17, 2015

    KULE KUSHOTO KWA OSCAR NI `JANGA`, KWA MSUVA!!!! KWELI MUNGU HAKUPI VYOTE.

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    Platnum Waliasisiwa kwa msaada wa Fedha za Dhahabu na baadaye ikamilikiwa na Jeshi. Hawana historia ya Kutisha katika Michuano ya kimataifa Lakini pia siyo timu ya Kubeza.
    Wawakilishi Pekee wa Tanzania Katika Michuano ya Kimataifa ( SHIRIKISHO) Yanga walikabiliana na Platnum Uwanja wa Taifa Dar Esa Salaam na Yanga ikaibuka na Ushindi `Mujarrab` wa mabao 5-1.
    Ni Ushindi Mzuri hasa kwakuwa ni uwanja wa Nyumbani unaokulazimu kuutumia Vyema katika michuano migumu kama hii.
    Niliushuhudia Mchezo huo kwa Dakika zote ingawa kuna wakati nilikuwa nikiangalia pembeni na kurejesha mato yangu Uwanjani.
    Oscar Joshua kulia dhidi ya mchezaji wa Platinum FC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Kidogo niliiona Yanga ikicheza kwa maelewano kuanzia safu ya Ulinzi,katikati na hata ushambuliaji tofauti na ilipokutana na Simba ( mpaka unajiuliza ilikuwaje???) na Ndiyomaana rafiki yangu mkubwa ambaye ni mpennzi wa Yanga Omar Abas wa Kule Arusha haishi kunipigia simu kila mara akihoji,,hivi yanga inafungwaje na Simba kaka?? Mbona inacheza vizuri sana ikikutana na timu nyingine??. Hata mimi sina jibu.
    Kuna aina ya Wachezaji wa Tanzania ambao wakikutana na wachezaji wenye uwezo mkubwa ama wenyekutumia akili unabaini mapungufu yao ama makosa yao wanayoyafanya mara kwa mara.
    Nianze na Mlinzi wa Kushoto wa Yanga na Taifa stars Osca Fannuel Joshua. Ni Mchezaji ambaye kwa Macho tu ukimwangalia katika Mchezo mmoja unabaini kuwa `huyu alianza kucheza soka ukubwani`.
    Ni Mchezaji asiyependa kukaa na mpira hata kama alipaswa kufanya hivyo kwa wakati huo, ni Mlinzi asiyepanda kuongeza mashambulizi hata kama alipaswa kufanya hivyo kwa wakati huo.
    NI aina ya mchezaji ambaye `moyo unakuenda mbio` kila akiwa na mpira katika Lango lake ( la Yanga) unahofia `anakosea! Anakosea! Ni Mchezaji asiyeaminika akiwa na mpira,wakati wowote anaweza kuupoteza .
    Osca Joshua amekuwa akitumia mguu wa kushoto ( ambao Ndiyo mguu wake kimpira) Linapokuja suala la kutumia mguu mwingine tofauti na Kushoto aliyozoweya inakuwa shida.
    Simon Msuva kulia akimtoka beki wa Polisi katika Ligi Kuu

    Ni Mchezaji aliyehishiwa `Control` na Ndiyo maana akipigiwa Mpira kutoka Mbali kisha akafanikiwa kuutuliza mpira huo huenda hatua tatu mbele yake. Jambo ambalo halipaswa kwa Mchezaji . Mchezaji anapaswa kuutuliza mpira na usiende mbali na himaya yake kwa maana ya hatua moja.
    Kwakila anayemtazama Osca atakubalia kuwa mara kwa mara huwa anapokonywa mpira anapokuwa jirani na adui kwakuwa mpira hautulii mguuni mwake.
    Mlinzi huyo `nisiyemuamini` akikutana na washambulizi wa pembeni wajanja,wenye kutumia akili zaidi mabao mengi yatatoka upande wake.
    Hivyo basi Yanga iendelee kumtumia Osca lakini itambue ni mchezaji mwenye mapungufu yatayoweza kuigharimu timu hiyo wakati wowote. Kule kwa Osca ni `janga` ipo siku mtaamini kwa msiyoamini.
    Nirejee kwa Mshambulizi wa Pembeni Simon Msuva.Msuva anatajwa kuwa ni mshambulizi hatari Tanzania .Ni Mshambulizi mwenye kasi, aliyekosa vitu Fulani vitakavyomfanya akawiye kucheza soka Ulaya.
    Kulikuwa hakuna haja ya kumleta mtu kama `Sherman` kama Msuva angekuwa na vitu ambavyo kwasasa hana ( nitataja)
    Msuva amekosa `akili` uwanjani. Naomba nieleweke vyema na ninarudia amekosa akili uwanjani. Ama akili ya Mpira. Inawezekana Msuva ana akili sana nje ya uwanja. Lakini akili hizo hatumii akiwa uwanjani,ama hana ama vyote viwili.
    Anaugua Ugonjwa kama wa Osca, pia amekosa `Control` kama Osca. Msuva ni aina ya Mchezaji aliyekosa malezi ya soka akiwa `mbichi`.
    Kinachomsaidia Msuva ni Mbiyo pekee. Lakini ujanja ama akili ya kufunga ama kuwapita walinzi kama siyo hana basi huwa hazitumii.
    Msuva ana umbo linalomfanya ateleze mbele ya walinzi,ana kasi lakini ugonjwa huo wa kukosa control na akili ya mpira vitamfanya akawiye bila kuvuka mipaka ya Nchi kucheza soka.
    Kwasababu hizo na Ndiyomaana kuna siku wanayanga hulalamika ama humlalamikia Msuva kucheza `Hovyo` na kuna siku humpigia makofi kwa kucheza vyema.
    Ni kwasababu Msuva anapokutana na Walinzi wanaomkaba kwa mbali na kumpa nafasi ya kutanguliza mpira na kukimbia basi Msuva lazima awe tishio siku hiyo.
    Lakini anapokutana na Walinzi wanaobaini mapungufu yake Msuva hulalamikiwa kucheza Hovyo.
    Hana akili ya pili au yatatu kutumia mbinu mbadala pale walinzi wanapobaini mbinu zake.
    Watanzania wataendelea kuona wachezaji hawa wenye `homa ya vipindi` kutokana na kukosa vitu kama hivyo.
    Kushoto kwa Yanga lolote laweza kutokea. Wingi ya Msuva amekosa mambo kadha ikiwamo akili ya soka. Na Ndiyomaana nasema Mungu hakupi kila kitu,ukikosa hiki utapata kile. Msuva kapewa Mbiyo tu.
    Pia nitoea angalizo kwa Yanga itakayosafiri kwenda Zimbabwe,ushindi wa mabao 5-1 ni mzuri lakini bado yanga haijaitoa Platnum.Lolote laweza kutokea.
    Sitoshangaa kama Mwamuzi akawapa Platnum penalty tatu,akatoa kadi mbili Nyekundu kwa wachezaji wa Yanga na akaweka filimbi mfukoni wachezaji wa Platnum wakiwa `off side`.
    Alafu Yanga wakarejea kama Azam wakilia `hujuma` . Namaanisha Yanga ijiandae pia kwa Hujuma kama hizo.Siyo mara moja ama mbili timu za Tanzania Zimetolewa kwa Mtindo huo.

    (Mwandishi wa makala haya ni mtangazaji wa Redio One na ITV na anapatikana kwa namba +255 655 250157 na +255 752 250157)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KULE KUSHOTO KWA OSCAR NI `JANGA`, KWA MSUVA!!!! KWELI MUNGU HAKUPI VYOTE. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top