KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kukutana Jumamosi (Aprili 14 mwaka
huu) kujadili rufani ya Yanga inayopinga kunyang’anywa pointi tatu.
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace
Wambura amesema leo kwamba Kamati ya Ligi ya TFF iliinyang’anya Yanga pointi
tatu ilizopata kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Coastal Union kwa
kumchezesha beki Nadir Haroub anayetumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.
Katika hatua nyingine, Wambura
amesema Kocha Kim Poulsen, leo (Aprili 10 mwaka huu) ametaja kikosi cha
wachezaji 21 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20
(Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa umri huo.
Kikosi hicho kimeingia kambini
leo (Aprili 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi dhidi ya
Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioitwa kwenye
kikosi hicho ni Saleh Ally Malande (Simba), Aishi Salum Manula (Azam), Hassan
Khamis Kessy (Mtibwa Sugar), Said Ruhava Samir (Falcon, Pemba), Carlos Protus
Kilenge (TSC Mwanza), Dizzana Issa Yarouk (Azam), Amani Peter Kyata (African
Lyon) na Issa Rashid Issa (Mtibwa Sugar).
Emily Mgeta Josiah (TSC Mwanza),
Khamis Jamal Mroki (Mtibwa Sugar), Ramadhan Suzana Singano (Simba), Frank James
Sekule (Simba), Frank Domayo Raymond (JKT Ruvu), Omega Sunday Seme (Yanga),
Abdallah Kilala Hussein (Falcon, Pemba) na Ibrahim Rajab Juma (Villa Squad).
Hassan Saleh Dilunga (Ruvu
Shooting), Alhaje Said Zege (JKT Ruvu), Jerome Lambele Reuben (Moro United),
Atupele Green Jackson (Yanga), Simon Msuvan Happygod (Moro United) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo).
Mechi ya marudiano dhidi ya
Sudan itachezwa jijini Khartoum kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.
Fainali za Afrika kwa vijana
zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria. Timu nne za juu kwenye fainali hizo
zitacheza Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini Uturuki kuanzia Juni hadi
Julai mwaka huu.



.png)
0 comments:
Post a Comment