|
Pichani, washambuliaji chipukizi
wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta wa pili kulia na Thomas Emmanuel Ulimwengu wa pili kushoto wakimkabidhi
Idriss Mbuyamba katikati yao, zawadi ya shindano linalondeshwa na klabu yao, Tout Puissant Mazembe
la ‘Picha ya Wa Zamani’ Jumamosi mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC). Mbuyamba alimwaga machozi kwa sababu ya Samatta, kutokana na
kutoamini macho yake baada ya kukutana na staa huyo, baada ya kushinda shindano hilo.
Sama Goal atarajea uwanjani wii hii, baada ya kupona bega aliloumia kwenye
mechi ya kwanza ya TP Mazembe dhidi ya Power Dynamos y Zambia mjini Kitwe
iliyoisha kwa sare ya 1-1. Mazembe iliitoa Dynamos kwa jumla ya mabao 7-1,
baada ya kuifunga 6-0 katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 32 Bora ya Ligi ya
Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki. Samatta ndiye aliyefunga bao katika sare ya
1-1 mjini Kitwe.
|
0 comments:
Post a Comment