![]() |
| Cheki Messi anavyotupia kitu kwenye nyavu |
MSHAMBULIAJI Lionel Messi amefunga
bao la 61 usiku wa kuamkia leo na kutoa pasi mbili za mabao, akiiongoza Barcelona
kuichapa Getafe 4-0 katika La Liga na kuwafanya mabingwa hao watetezi sasa
wazidiwe pointi moja tu na vinara wa Ligi ya Hispania, Real Madrid.
Messi aligongeana vizuri mno na Andres
Iniesta kabla ya kufunga dakika ya 44. Messi sasa anaongoza kufunga mabao
katika La Liga akiwa ana mabao 39, bado moja tu kufikia rekodi aliyoweka Cristiano
Ronaldo msimu uliopita.
Messi amefunga mabao 12 katika
mechi zake 13 zilizopita, akifanya jumla ya mabao 24.
Ni mchezaji wa kwanza kufikisha
mabao 60 katika ligi kubwa za Ulaya, tangu mshambuliaji wa zamani wa Bayern
Munich, Gerd Mueller alipofikisha mabao 67 msimu wa 1972-73.
Alexis Sanchez alifunga dakika
ya 13 na 73 na Pedro Rodriguez akafunga
dakika ya 75, wakiiwezesha Barcelona kushinda mechi ya 10 mfululizo ya ligi.
Real Madrid inaweza kurejesha
pengo la pointi nne dhidi ya Barca, iwapo itashinda mechi yake ya leo dhidi ya Atletico
Madrid.



.png)
0 comments:
Post a Comment