![]() |
| Wachezaji wa Liverpool wakimpongeza Andy Carroll |
BLACKBURN, England
MSHAMBULIAJI Andy Carroll alifunga
bao kwa kichwa katika dakika ya kwanza ya dakika za majeruhi na kuiwezesha
Liverpool kushinda 3-2 dhidi ya Blackburn iliyo hatarini kushuka daraja.
Lakini Liverpool ilimpoteza wake
mwingine, aliyesimamishwa kuelekea Nusu Fainali ya Kombe la FA mwishoni mwa
wiki hii dhidi ya Everton.
Mabao ya Maxi Rodriguez dakika
ya 13 na 16 yaliwafanya Wekundu wa Anfield waongoze 2-0.
Kipa wa Liverpool, Alexander
Doni, aliyechukua nafasi ya Pepe Reina anayetumikia adhabu, alipewa kadi nyekundu
ya moja kwa moja kwa kumuangusha Junior Hoilett kwenye eneo la hatari dakika ya
25.
Kipa aliyetokea benchi, Brad
Jones alizuia mkwaju wa penalti wa Ayegbeni Yakubu dakika ya 27, lakini Yakubu akafunga
mabao mawili dakika za 36 na 61 na kufanya 2-1.
Penalti aliyopiga baadaye
ilimfanya atomize mabao 16.
Jones alikuwa mwenye bahati kwa
kutotolewa nje kwa kadi nyekundu, baada ya kumsukuma Yakubu kwenye eneo la
hatari.
Liverpool ni ya nane sasa kwa
pointi zake 46, wakati Blackburn ni ya 18 nyuma ya Queens Park Rangers kwa
tofauti ya mabao.



.png)
0 comments:
Post a Comment