MBIO za Manchester United kufukuza taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, zimepunguzwa kasi jioni hii na Everton waliopigana kutoka nyuma kwa mabao 4-2 na kutoa sare ya 4-4 kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Wayne Rooney alifunga bao dakika ya 41 akiunganisha krosi ya Nani kusawazisha bao, baada ya Nikica Jelavic kuwafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 33.
Danny Welbeck na Nani wakafunga mabao mawili kabla ya Marouane Fellaini kufunga kwa upande wa Everton.
Rooney alifunga bao lililoelekea kuwa la ushindi, lakini Everton wasawazisha mawili ndani ya dakika tatu kupitia kwa Jelavic na Steven Pienaar.
Sasa Man United iko kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi, dhidi ya Manchester City ambao watamenyana na  Wolves baadaye.

VIKOSI, KADI ZA NJANO (3) NA WALIOWAPISHA WENGINE (4)

Manchester United

  • 01 De Gea
  • 03 Evra Booked
  • 05 Ferdinand
  • 06 Evans
  • 21 Rafael
  • 16 Carrick
  • 17 Nani
  • 22 Scholes (Jones - dk86' )
  • 25 Valencia (Hernandez -dk 89' )
  • 10 Rooney
  • 19 Welbeck

BENCHI

  • 40 Amos
  • 04 Jones
  • 12 Smalling
  • 11 Giggs
  • 13 Park Ji-sung
  • 18 Young
  • 14 Hernandez

Everton

  • 24 Howard
  • 02 Hibbert
  • 05 Heitinga
  • 06 Jagielka
  • 15 Distin Booked (Cahill - dk83' )
  • 18 Neville Booked
  • 04 Gibson
  • 21 Osman (McFadden - dk63' )
  • 22 Pienaar
  • 25 Fellaini
  • 07 Jelavic

BENCHI

  • 01 Mucha
  • 17 Cahill
  • 20 Barkley
  • 11 Stracqualursi
  • 14 McFadden
  • 19 Gueye
  • 28 Anichebe
Refa: Jones
Mahudhurio: 75,522

TAKWIMU ZA MECHI


KUTAWALA MCHEZO48%52%96minManchester UnitedEverton
MASHUTI
2017


11
1
0
KONA
52

FAULO

811