![]() |
| Iniesta akiwa haamini macho yake |
KIUNGO wa Barcelona, Andres Iniesta amesema kwamba kipigo
cha jana katika Clasico kimewaumiza sana mioyo yao, lakini ameahidi vijana wa
Pep Guardiola wataibuka katika mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa
dhidi ya Chelsea.
Wakatalunya hao waliingia kwenye mchezo huo kwa matumaini ya
kupunguza pengo la idadi ya pointi wanazozidiwa na Los Blancos kileleni mwa La Liga
na kubaki moja, lakini sasa wanaachwa pointi saba baada ya kulala 2-1 Camp Nou,
Cristiano Ronaldo akiifungia bao la ushindi timu yake dakika ya 73, dakika tatu
tangu Alexis Sanchez aisawazishie Barca, kufuatia Sami Khedira kufunga la
kuongoza mapema.
Real sasa wanahitaji sare moja na kushinda mechi moja katika
mechi nne zilizobaki ili kutangaza ubingwa na hata Iniesta amesema anafikiri
mbio za ubingwa sasa zimkwisha Hispania.
“Imetuumiza miyo yetu kutokuwa tena kwenye mbio za taji la
La Liga, lakini tukubali,” alisema kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania na
kuongeza; “Taji la La Liga dhahiri limetuponyoka. Tofauti ni kubwa kwenye
pointi na mechi zilizobaki ni chache.
"Tulijua itakuwa ngumu, hususan kutokana na kutambua
kwamba wanajitegemea wao wenyewe – lakini tumeacha liende.
“Suluhisho pekee kwetu lilikuwa ni ushindi, na walicheza na
hilo akilini mwao. Kwa sare, wakati ilipoonekana kuwa ngumu, tulipigania ushindi,
walitumaliza haraka sana.”
Iniesta, pamoja na hayo hana shaka Barca itasahau kuhusu
kipigo cha Clasico na kuingia vitani tena kujaribu kuupiku ushindi wa 1-0 wa
Chelsea kwenye mchezo wa kwanza kwao.
"Tunatakiwa tujiandae na tuwe sawa kwa ajili ya mechi
ya Jumanne," alisema mshindi huyo wa Kombe la Dunia.
"Tunataka kuelekeza fikra zetu katika mashindano mengine.
Maji yakishamwagika, hayazoleki.
Ni mchezo tofuti kabisa dhidi ya Chelsea. Kipi tunafikiria
ni kuhusu kuingia Fainali ya Ligi ya Mabigwa.”



.png)
0 comments:
Post a Comment