bongostaz.blogspot.com.
Mapigo ya moyo ya Muamba yalisimama kwa dakika 78 mwezi
uliopita katika Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham, lakini na kutoka
hospitali mapema wiki hii.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, Muamba amesema leo na
kunukuliwa na gazeti la The Sun la Uingereza kwamba, 'hakusikia maumivu kabisa''
kabla ya kuzimia, zaidi ya kuanza kusikia kizunguzungu.
Alisema: ''Nilihisi nalegea na mwili kupoteza nguvu kabla ya
kuanguka, kichwa changu kikiangukia uwanjani mbele yangu, kasha ndivyo ikawa hivi.
Giza, hakuna kitu.''
Muamba alisema 'kwa dakika 78 nilikuwa mfu na hata kama
nimepona, ilitarajiwa nitakuwa na matatizo ya ubongo, lakini niko hai sana.'



.png)
0 comments:
Post a Comment