• HABARI MPYA

    Friday, May 10, 2024

    TASWA KUWAFUNDA WAANDISHI CHIPUKIZI NCHINI


    CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatarajiwa kuendesha mafunzo kwa waandishi wa Habari wanaochipukia katika nchi mbalimbali nchini.
    Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu TASWA, Imani Makongoro imesema kwamba lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari za Michezo chipukizi katika Nyanja mbalimbali – ili waweze kutekeleza vyema majukumu yao, ikiwa ni sehemu ya maelekezo ya Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), kinachotaka vyama vya kila nchi viwe na programu hizo.
    Kutokana na hali hiyo TASWA inawajulisha kuwa Awamu ya Kwanza ya Mafunzo hayo itahusisha waandishi wa habari chipukizi wanaofanya kazi kwenye vyombo vya habari za kidigitali, ambao umri wao haupungui miaka 18 na hauzidi miaka 30 na yatasimamiwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Egbert Mkoko pamoja na baadhi ya wanahabari wakongwe wa habari za michezo nchini.
    TASWA inawaomba wanahabari wote chipukizi wa habari za kidigitali, kama kuna anayetaka kushiriki mafunzo hayo awasiliane na Naibu Katibu Mkuu wa TASWA, Imani Makongoro kwa email: taswatz@yahoo.com, mhusika aeleze majina yake kamili, jinsia, umri, chombo anachofanyia kazi, kiwango chake cha elimu na mkoa aliopo. Mwisho wa kupokea maombi ni Mei 25, 2024. Waandishi chipukizi wa magazeti, redio na televisheni utaratibu wao utafuata.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TASWA KUWAFUNDA WAANDISHI CHIPUKIZI NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top