• HABARI MPYA

    Thursday, May 23, 2024

    MABINGWA YANGA WAHUDHURIA BUNGE LA BAJETI YA MICHEZO DODOMA


    MABINGWA wa Tanzania,Yanga SC leo wamehudhuria Bunge la Bajeti na kumshuhudia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Daniel Ndumbaro leo akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha wa 2024/25.
    Mapendekezo ya jumla yaliyowasilishwa na Waziri, Wakili Dk. Ndumbaro ni zaidi ya Sh. Bilioni 285.3, ambayo ni ongezeko la Sh. Bilioni 250 na ushei kutoka bajeti ya mwaka jana ya Sh. Bilioni 35 na zaidi.
    Katika mapendekezo hayo, Waziri huyo ameomba Sh. Bilioni 258 na zaidi kwa ajili ya Gharama za Maendeleo, ambayo ni ongezeko la zaidi ya Sh. Bilioni 248 kutoka za mwaka jana Bilioni 9, Sh. Bilioni 11 kwa ajili ya matumizi ya kawaida (Mishahara nk) na Sh. Bilioni 15 kwa matumizi mengineyo. 
    Baada ya uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Bajeti hiyo, Naibu Spika, Mussa Azzan ‘Zungu’ aliwatambulisha wageni mbalimbali waalikwa katika kikao cha leo – akianza na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Ally Said,viongozi wenzake, Kocha Muargentina Miguel Gamondi na wachezaji. 
    Aidha, Naibu Spika, Mussa Azzan ‘Zungu’ alimtambulisha pia Mkurugenzi wa Wanachama wa Simba SC, Hamisi Kisiwa na wageni wengine.
    Akitoa mchango wake juu ya Bajeti hiyo, Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato David Chumi aliipongeza Azam TV kwa kuonyesha matukio makubwa ya kimichezo ya Kitaifa na Kimataifa na hata ya nchi jirani – na jkutoa ushaur kwa Serikali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABINGWA YANGA WAHUDHURIA BUNGE LA BAJETI YA MICHEZO DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top