TIMU ya Arsenal imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora UEFA Europa League baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Benfica jana Uwanja wa Georgios KaraiskákiJijini Piraeus.
Arsenal inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang mawili dakika ya 21 na 87 na Kieran Tierney dakika ya 67, wakati ya Benfica yamefungwa na Diogo Gonçalves dakika ya 43 na Rafa Silva dakika ya 61.
0 comments:
Post a Comment