• HABARI MPYA

    Saturday, December 17, 2016

    TFF YAPATA MKURUGENZI MPYA WA FEDHA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemteua Aziza Badru Mwanje kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala kuanzia Januari Mosi, 2017. 
    Uteuzi huo umefanywa leo (Desemba 17, 2017) na Kamati ya Utendaji ya TFF kufuatia mchakato wa usaili uliohusisha waombaji wengine wawili na kufanywa na Bodi ya Ajira ya TFF.
    Aidha, Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko ya wajumbe katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambapo Wakili Patrick Sanga atakuwa Makamu Mwenyekiti wakati Mwenyekiti anaendelea kuwa Wakili Richard Sinamtwa.
    Wajumbe wengine walioongezwa kwenye Kamati hiyo ni Adam Mihayo na Hassan Hassanoo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA). 
    Wakili Raymond Wawa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kuziba nafasi ya Joseph Mapunda ambaye ameomba kupumzika, wakati Mia Mjengwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAPATA MKURUGENZI MPYA WA FEDHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top