• HABARI MPYA

    Monday, March 16, 2015

    MERREIKH WAWACHAPA WAANGOLA 2-0, MAZEMBE YAPIGWA 1-0 SAUZI

    WABABE wa Azam FC katika michuano ya Afrika, El Merreikh ya Sudan juzi wameanza na ushindi wa 2-0 katika mchezo wa kwanza, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati TP Mazembe ya DRC ilifungwa 1-0 na Mamelodi Sundowns nchini Afrika Kusini.
    Merreikh iliyoitoa Azam FC kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa Dar es Salaam 2-0 na kwenda kushinda Khartoum 3-0, sasa inatakiwa kwenda kuulinda ushindi huo ugenini ili isonge mbele.
    Mazembe, yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu inatakiwa kushinda 2-0 nyumbani ili kusonga mbele.    
    Mbwana Samatta kushoto na Thomas Ulimwengu kulia wanaochezea TP Mazembe

    Katika mechi nyingine za kwanza, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika juzi, Kaizer Chiefs ilifungwa 1-0 nyumbani Afrika Kusini na Raja Casablanca ya Morocco, MC El Eulma ilitoka 0-0 na Asante Kotoko, Real Banjul imetoka 1-1 na ES Setif, Coton Sport imetoka sare ya 0-0 na S.M Sanga Balende, Mangasport imefungwa 3-1 nyumbani na Stade Malien na APR FC imefungwa 2-0 nyumbani na Al Ahly ya Misri na Zesco United
    imelazimishwa sare ya  1 – 1 AS Kaloum
    katika mechi za jana El Hilal ya Sudan imeifunga 4 – 0 Big Bullets ya Malawi, U.S.M Alger imeichapa 5 – 1 Pikine, AC Semassi imepigwa 5- 0 Club Sportif Sfaxien, Enyimba FC imeifunga 1-0 Smouha, Cosmos Bafia imefungwa 1-0 nyumbani na Esperance na Gor Mahia ya Kenya imefungwa 0-1 nyumbani na AC Leopards  ya Kongo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MERREIKH WAWACHAPA WAANGOLA 2-0, MAZEMBE YAPIGWA 1-0 SAUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top