BAO pekee la Jordan Henderson dakika ya 68 limetosha kuipa Liverpool ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji Swansea Uwanja wa Liberty usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Wekundu wa Anfield sasa wanafikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 29, ingawa wanabaki nafasi ya nne nyuma ya mahasimu, Manchester United wenye pointi 56, Arsenal 57, Manchester City 58 zote zikiwa zimecheza mechi 29, wakati vinara Chelsea wana pointi 64 za mechi 28.
Kikosi cha Brendan Rodgers hakijaruhusu nyavu zake kutikiswa katika mechi sita zilizopita za Ligi Kuu na Jumapili wiki hii wanaikaribisha Manchester United Uwanja wa Anfield.
Kikosi cha Swansea kilikuwa: Fabianski, Naughton, Amat, Williams, Taylor, Ki/Dyer dk80, Cork, Shelvey, Gomis, Sigurdsson/Emnes dk89 na Routledge/Montero dk73.
Liverpool: Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Lallana/Johnson dk88, Henderson, Allen, Moreno/Gerrard dk64, Sterling, Sturridge na Coutinho.
Jordan Henderson akishangilia baada ya kuifungia Liverpool bao pekee la ushindi jana
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2997795/Swansea-0-1-Liverpool-Jordan-Henderson-s-deflected-goal-earns-Brendan-Rodgers-Reds-vital-victory-race-four-berth.html#ixzz3UbyRGry8


.png)
0 comments:
Post a Comment