![]() |
| Havelange |
MADAKTARI wamesema rais wa
zamani wa FIFA, Joao Havelange anaendelea vizuri baada ya kupatiwa tiba makini
ya matatizo ya moyo, kufuatia kurejeshwa chumba cha wagongwa wanaostahili
uangalizi makini katika hospitali anayotibiwa nchini Brazil.
Madaktari wamesema babu huyo wa
umri wa miaka 95, Havelange ianapata nafuu kutoka matatizo yake ya moyo ambayo
yalimfanya awe taabani katika hospitali ya Samaritano, ambako alilazwa kwa
zaidi ya wiki tatu baada ya athari zilizogundulika katika kifundo cha mguu wake
wa kulia.
Dk. Joao Mansur Filho amesema Havelange
atakuwa sawa haraka iwezekanavyo.
Havelange alikuwa rais FIFA kuanzia
1974-1998. Alistaafu katika kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) mwishoni mwa
mwaka jana kwa sababu za kiafya.



.png)
0 comments:
Post a Comment