• HABARI MPYA

    Friday, March 29, 2024

    SIMBA CHALI KWA MKAPA, WAPIGWA 1-0 NA AHLY KINDA WA MIAKA 22


    MABINGWA watetezi, Simba SC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Simba SC katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Bao pekee la Al Ahly katika mchezo huo limefungwa na kiungo mwenye umri wa miaka 22 tu, Ahmed Koka dakika ya nne tu na timu hizo zitarudiana Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri.
    Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali.
    Ikumbukwe timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA CHALI KWA MKAPA, WAPIGWA 1-0 NA AHLY KINDA WA MIAKA 22 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top