MABAO ya Sadio Mane dakika ya 31 na Thiago Alcantara dakika ya 90 jana yaliipa Liverpool ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
Kwa ushindi huo, Liverpool imefikisha pointi 57 na kusogea nafasi ya sita, ikizidiwa pointi moja na West Ham United baada ya wote kucheza mechi 34, wakati Southampton inabaki na pointi zake 37 za mechi 34 pia katika nafasi ya 16.
0 comments:
Post a Comment