• HABARI MPYA

    Thursday, May 06, 2021

    CHELSEA YAITOA REAL MADRID, YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA

     WENYEJI, Chelsea wamefanikiwa kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Real Madrid usiku wa Jumatano Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
    Mabao ya Chelsea yamefungwa na Timo Werner dakika ya 28 na Mason Mount dakika ya 85 na kwa matokeo hayo, The Blues inatinga fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Jijini Madrid.
    Sasa Chelsea itakutana na Manchester City katika fainali ya timu za England tupu Mei 29 Uwanja wa Atatürk Olimpiyat Jijini İstanbul nchini Uturuki.


    Manchester City yenyewe imefika fainali baada ya kuitoa PSG ya Ufaransa kwa jumla ya 4-1, ikishinda 2-1 Paris wiki iliyopita na 2-0 Uwanja wa Etihad jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAITOA REAL MADRID, YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top