• HABARI MPYA

    Saturday, May 08, 2021

    UONGOZI WA YANGA SC WAPINGA MCHEZO DHIDI YA SIMBA SC KUHAMISHIWA USIKU, WADAI NI UKIUKWAJI WA KANUNI

    UONGOZI wa Yanga SC umepinga mchezo wao Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya watani wa jadi, Simba uliokuwa uanze Saa 11:00 iioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kusogezwa mbele hadi Saa 1:00 usiku kwa agizo la Serikali.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mchana huu imesema kwamba wamepokea agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuisogeza mbele mechi hiyo hadi Saa 1:00 usiku.
    Lakini Yanga SC wamesema kwamba kufanya hivyo ni kukiuka kanuni inayotaka mchezo ubadilishwe muda sio chini ya Saa 24 kabla.


    Mchezo huo marudiano wa msimu baada ya miamba hiyo kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Novemba 7, mwaka jana utaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya AzamSports1HD ya Azam TV.
    Mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa, Yanga SC walitangulia kwa bao la penalti la mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kipindi cha kwanza, kabla ya beki Mkenya, Joash Onyango kuisawazishia Simba mwishoni kipindi cha pili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UONGOZI WA YANGA SC WAPINGA MCHEZO DHIDI YA SIMBA SC KUHAMISHIWA USIKU, WADAI NI UKIUKWAJI WA KANUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top