• HABARI MPYA

    Tuesday, July 01, 2014

    DI MARIA AIPELEKA ARGENTINA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA

    ZIKIWA zimesalia dakika mbili mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti baada ya Argentina na Uswisi kuwa hazijafungana katika mchezo wa 16 Bora Kombe la Dunia jioni hii Brazil, Angel di Maria alifanya mambo.  
    Nyota huyo wa Real Madrid aliitendea haki pasi nzuri ya Lionel Messi wa Barcelona dakika ya 118 kuipeleka Argentina Robo Fainali ya Kombe la Dunia.
    Tofauti na ilivyotarajiwa akina Messi wangefuzu kiulaini, Uswisi waliibana Argentina na ilibaki kidogo mshindi aamuliwe kwa matuta.   
    Kikosi cha Argentina kilikuwa; Romero, Federico Fernandez, Zabaleta, Garay, Rojo/Basanta dk105+1, Gago/Biglia dk106, Mascherano, Di Maria, Higuain, Messi na Lavezzi/Palacio dk74.
    Uswisi; Benaglio, Lichtsteiner, Schar, Djourou, Rodriguez, Inler, Behrami, Xhaka (Fernandes 66), Shaqiri, Mehmedi/Dzemaili dk113 na Drmic/Seferovic dk82.
    Maajabu: Angel di Maria akishangilia baada ya kuifungia Argentina bao la ushindi
    Embrace: Lionel Messi was the architect of the goal
    Lionel Messi akimpongeza di Maria
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DI MARIA AIPELEKA ARGENTINA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top