KOCHA MPYA COASTAL UNION AAHIDI STAREHE KWA WAGOSI
Kocha mpya wa Coastal Union ya Tanga, Yussuf Chipo akizungumza na Waandishi wa Habari leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam baada ya kutambulishwa. Chipo anayerithi mikoba ya Hemed Morocco aliyeondolewa, ameahidi kuifanya Coastal Union kuwa tishio katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment